
KAMPUNI maarufu ya kutengeneza Saruji, Mbeya Cement yenye makazi yake Makuu jijini Mbeya, imeamua kuuza ofisi na mali zake zote zilizokuwa kwenye ofisi yao iliyopo maeneo ya Tazara jijini dar es Salaam.

Mbeya Cement imeipa idhini Kampuni ya Highland Auction Mart kusimamia mnada wa hadhara wa mauzo ya vifaa vyote vilivyomo ndani ya ofisi hiyo.
Akizungumza na Global TV Online, Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Highland Auction Mart, Falcom Mlelwa amesema mnada huo utafanyika leo Ijumaa, januari tatu kuanzia saa 7:00 mchana kwenye ma-godown ya Tazara (zilipokuwa ofisi hizo).

“Vifaa vitakavyouzwa ni fenicha zote za ofisini, meza, viti, self za kutunzia fedha, vifaa vya computers na computers, servers, routers, CPU, UPS na vingine vingi. Pia, vitauzwa vitu chakavu kama mabomba, matanki ya maji na mafuta.

“Mbali na hivyo, kutakuwa na makontena tupu yenye ukumbwa wa aina tofauti. Hii ni kwa idhini iliyotolewa na mbeya cement ambao wameamua kuuza vifaa vyake, wananchi wote mnakaribishwa sana kesho Januari 3,” amesema Mlelwa.
Kwa mawasiliano zaidi piga simu namba 0788 373 022 au 0759 670230.