
KIONGOZI wa kanisa katoliki Duniani Papa Francis amesihi Marekani na Iran wakae kwenye meza ya majadiliano ili wapate suluhu ya mgogoro uliopo baina yao.

Papa ameyasema hayo katika hotuba yake iliyochukua dakika 50 akiwa Vatican na kuongeza kuwa mwaka jana ulikuwa na matukio mengi mabaya ambayo asingependa kuyaskia tena, kama vita, Xenophobia pamoja uharibufu wa hali ya hewa duniani.
Hii imekuwa mara ya kwanza kwa kiongozi huyo kuzungumza juu ya mgogoro huo mkubwa duniani.