NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, Ramadhan Kailima, amewasili makao makuu ya Taasisi ya Kupambana na Kupiga Vita Rushwa (TAKUKURU) Dodoma majira ya saa 8:50 asubuhi kwa ajili ya kuhojiwa akiwa na gari ya Land Cruiser T830 DNL.
Kailima alikwepa kuingilia lango kubwa la mapokezi, akaingilia lango dogo la moja kwa moja hadi chumba cha mahojiano ili kukwepa kamera za wanahabari.
Kiongozi mwingine anayetarajiwa kuhojiwa leo ni Naibu waziri wa Mambo ya ndani Hamad Masauni ambaye atawasili katika ofisi hizo za TAKUKURU saa sita mchana.
Wengine waliohojiwa jana Ijumaa, Januari 31, 2020, na Takukuru ni aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Kangi Lugola, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Balozi Mteule, Meja Jenerali Jacob Kingu na aliyekuwa Kamishna Jenerali wa Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye.
Kuhojiwa kwa watumishi hao ni utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli kuhusu mkataba tata wa zaidi ya Tsh trilioni 1 kwa walioingia na kampuni ya Romania kwa ajili manunuzi ya vifaa vya zimamoto.
View this post on Instagram

