MSANII wa Hip-hop nchini Marekani, Bashar Barakah Jackson maarufu Pop Smoke (20), amefariki baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana waliomvamia nyumbani kwake.
Polisi wamethibitisha tukio hilo na hadi sasa hakuna aliyekamatwa.
Smoke aliuawa jana Jumatano Februari 19, 2020, katika mazingira yanayooenaka kama uvamizi akiwa nyumbani kwake mjini Hollywood Hills.
Mwanamuziki huyo amewahi kufanya kazi na Nick Minaj na Travis Scott na alikuwa anapewa nafasi ya kufanya vizuri katika muziki wake.
