×

Saba Wafariki Kwa Ajali Morogoro (Picha +Video)

WATU saba wamefariki katika ajali iliyohusisha magari matatu iliyotokea eneo na Nanenane mkoani Morogoro usiku wa kuamkia leo Jumanne Juni 22, 2021.

 

Magari hayo ni Toyota Coaster, Cresta na lori la kampuni ya Dangote ambapo Coaster hilo lililogonga gari dogo na kisha kugongana na lori.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fortunatus Muslim amesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa Coaster kutaka kulipita gari dogo na kupoteza mwelekeo.

Katika ajali hiyo majeruhi walikimbizwa hospitali ya rufaa Mkoa wa Morogoro kwa matibabu.

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Albert Msando amewataka madereva kufuata kanuni na sheria za barabarani, akiwaasa abiria kuchukua tahadhari hasa wanapoona mwendo wa dereva hauridhishi ili kuepuka ajali kama hizo zinazopoteza nguvu kazi ya Taifa.

 

Kaimu mganga mfawidhi hospitali ya rufaa mkoani humo, Dk Messy Mgalawa alitaja idadi ya majeruhi na vifo akibainisha waliowapokea ni 24 na vifo saba.

 

 

Leave a Comment