
Dar es Salaam Februari 15, 2020: Kili Canvas iliyozinduliwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia Bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager hivi karibuni jijini Dar es Salaam, imekuwa kivutio kikubwa kwa wakimbiaji mbalimbali wa mji wa Moshi Mkoanj Kilimanjaro.
Canvas hiyo yenye lengo la kuhamasisha wakimbiaji wa vitongoji mbalimbali wa Mkoa wa Kilimanjaro katika kuelekea kilele cha mbio za Kili Marathon zinazotarajiwa kufanyika Machi Mosi, 2020 mkoani Kilimanjaro
Kili Canvas ni picha maalumu iliyochorwa kwa ukubwa ambapo mkimbiaji yeyote akipita karibu yake anapigwa picha na picha hiyo yenye muunganisho wa teknolojia ya kisasa baadaye kumtumia picha hiyo kupitia simu yake ya mkononi. Hata hivyo mkimbiaji anatakiwa kujisajili na kupewa chip maalumu ambayo anatakiwa kuwanayo kwa maelekezo ya wahusika.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Primium Lager, Pamela Kikuli alisema baada ya shamra shamra za maandalizi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam Kili Canvas sasa itakuwa Mkoani Kilimanjaro Manispaa ya Moshi Mjini ambapo wakazi wa Kilimanjaro watapata fursa ya kupigwa picha kwa teknojia maalumu ya kisasa kisha kutumiwa kwenye simu yako ikiwa ni sehemu ya kukuhamasisha wewe mkimbiaji na wakimbiaji wengine kujiandaa na kilele cha Mbio za Kili Marathon amzazo kilele chake ni Machi Mosi 2020.

Pamela alisema zaidi ya Nchi 52 Duniani baadhi ya wananchi wake wamejiandikisha kushiriki kilele cha mbio hizi, ni vyema basi kama watanzania na waandaaji wa mbio hizi tukawa mstari wa mbele kuhamasishana kushiriki kilele cha mbio hizi za Kili Marathon ambazo kwa mwaka hufanyika mara moja tu.
Kitenge alisema mwaka jana nilikimbia Kili Marathoni lanini mwaka huu pia lazima nishiriki pia kwa kuvuna record yangu yam waka jana.Si mimi tu bali wanafamilia wote wa Wasafi Jogging tunatarajia kushiriki Kili Marathon 2020.
“Mkoani Kilimanjaro Kili canvas itakuwa Mtaa wa Kilimanjaro Avenue kwa Jumatatu, Jumanne na Jumatano, Mtaa wa Seketure Kili canvas itakuwepo Alhamis na Ijumaa, Jumamosi Canvas itakuwa ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Jumapili Uwanja wa Ushirika Moshi ambapo kilele cha mbio hizo zitafanyika”, alisema Kikuli.
“Hii ni fursa kwa kila mtu anayependelea mchezo wa kukimbia, na si lazima awe ni mshiriki wa Kili Marathon, ndiyo maana tukasema yeyote anaweza kujisajili na kupata chip hiyo kwa kipindi hiki cha kuhamasishana kuelekea kilele cha mbio za Kili Marathon”.
