
Hospitali nchini zimetakiwa kubuni mbinu mbadala ya kujiendesha ili kuweza kuendelea kutoa huduma bora za kiafya badala ya kusubiri msaada kutoka serikalini.
Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Mbulu iliyoko mkoani Manyara mweshimiwa Chelestino Mofuga katika shehere ya miaka 64 ya Hospitali ya rufaa ya Kilutheri ya Haydom tangu ilipoazishwa na Wamisionari kutoka nchini Norway mwaka 1955 ambapo ilienda sambamba na uzinduzi wa mashine ya mpya ya CT Scan,Digital X-Ray,mashine ya kuchoma taka hatarishi na mashine ya Oxygen katika hospitali iyo.
Amesema ni vyema kwa viongozi wa hospitali mbali mbali nchini kubuni mbinu mbadala ya kuongeza vifaa tiba katika hospitali zao badala ya kusubiri mpaka msaada itoke serikali kwani kwa kufanya ivyo itawafanya kuendelea kutoa huduma bora na za haraka za kiafya kwa wagonjwa.

Ameipongeza uongozi wa hospitali ya Kilutheri ya Haydom kwa kubuni mbinu Mbadala ya kufanya changizo kwa wadau mbali mbali nchini na nje ya nchi kupitia mbio za riadha za Haydom Marathon ili kupata fedha za kununua mashine ya CT Scan na vifaa tiba zingine na kuongeza kuwa serikali iko nao bega kwa bega kuhakikisha wanashirikiana ili kuendelea kutoa huduma bora na ya garama nafuu kwa Watanzania wanaoishi vijijini.
Mwakilishi wa balozi wa Norway nchini Tanzania mweshimiwa Britt Hilde Kjolas amesema anafurahi kuona Watanzania wanaongoza hospitali ya Haydom kuwa na uweledi mkubwa na kufanya mambo makubwa ambayo kwake ni faraja na kuweka wazi kuwa wataendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuhakikisha sekta ya afya inapiga hatua kuliko ilivyo sasa.
Alisema ni jambo jema kuona vifaa vipya vimenunuliwa ambavyo nitaenda kuwasaidia wagonjwa ambao wengi wao ni wa vijijini na wenye kipato cha chini ivyo yale ambayo wamekuwa wakiyakusanya na kuyapigia debe yametokea na kuwa mambo mazuri.

Naye mkurugenzi mkazi wa shirika la NCA hapa Tanzania Gwen Bwerge ameshukuru kwa kuwa sehemu ya kuiwezesha Haydom kuwa ilipo na kuwa sehemu ya mpango mkuu wa uwezeshaji wa mpango wa upatikanaji wa huduma Tanzania chini ya sera ya huduma za afya kwa wote ambayo pia ni mpango ambao NCA kwa kushirikiana na serikali wameweka kuhakikisha ifikapo mwaka 2025 Watanzania wote wawe na uwezo wa kupata huduma za afya.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa tiba hospitali ya rufaa ya Kilutheri ya Haydom Dkt.Emmanuel Q.Nuwass amesema hospitali iyo itaendelea kutoa huduma za afya kwa kuzingatia Sera na miongozo ya wizara ya Afya,kwa kushirikiana na serikali ,na wadau wengine ili kuimarisha vita dhidi ya maradhi na umaskini.
Amesema kama uongozi wanamshukuru raisi Mh.Dr.John Pombe Magufuli,kwa kufanya maboresho na uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya nchini hasa mapato ya ndani na kwa kushirikiana na sekta binafsi.
Amesema katika kuboresha huduma za afya katika hospitali yao waliweza kushirikiana na wadau wa ndani na nje ya nchi kutafuta fedha kutoka vyanzo mbali mbali kwa malengo mahususi ya kununua vifaa tiba vipya na kuweka wazi kuwa njia iliyotumika ni kufanya mbio za hisani ya Haydom Marathon mwaka 2018 ambapo walifanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi milioni 107.
Amesema mbali na mbio waliweza kuwashirikisha wadau wao wakuu NORAD na NCA ambao walichangia shilingi bilioni 1.1 wakati FoH wakichangia karibu milioni 285 lakini fedha zikingine zikatolewa na serikali, KKKT Dayosisi ya Mbulu,watumishi wa hospitali (na HIHS,4CCP),wafanya biashara wa Haydom na nje ya Haydom na taasisi mbali mbali wakiwemo wadau wengine wa ndani ya nchi waliochangia kiasi cha shilingi milioni 185 na kufanikiwa kupata kiasi cha shilingi bilioni 1.55 ambazo zimetumika kununua vifaa tiba.
Amezitaja vifaa ivyo kuwa ni CT Scan toka kampuni ya Siemens,brand ya Somato GO NOW,IVR Technology, slices 32 yenye thamani ya shilingi milioni 654.2 ikiwa imeshawahudumia zaidi ya wagonjwa 250,mashine ya pili ni Digital X-Ray kutoka kampuni ya GE Healthcare,model ya CR6000 50kw yenye detector mbili thamani yake ikiwa ni shilingi milioni 320.2.
Mashine ya tatu ni mtambo wa kuzalisha hewa ya Oxsijeni kwa ajili ya wagonjwa (Oxygen plant) kutoka kampuni ya Ozcan Kardelser aina ya PSA 300 yenye thamani ya shilingi milioni 372.9 ambayo ina uwezo wa kuzalisha mitungi yenye mita za ujazo 8.5 kuanzia 40 hadi 56 kwa siku.ikiwa imezalisha mitungi 1665 na kuokoa kiasi cha shilingi milioni 72 kilichokuwa kinatumika kununulia.
Mashine ya mwisho ni kuteketeza taka hatarishi zinazozlishwa hospitalini ,model yake ni KRWM 100 yenye uwezo wa kuchoma taka 100kg kwa saa katika nyuzi joto 1200 ambayo imegarimu shilingi milioni 203.
Dokta Nuwasse ameongezea kuwa pamoja na ununuzi wa vifaa hivyo lakini pia wamejenga na kukarabati majengo kwa ajili ya vifaa hivyo na kuweka wazi kuwa maeneo ambayo yalikarabatiwa ni jengo la idara ya mionzi (Radiology), jengo la mtambo wa kuzalisha oksijeni,na kujenga jengo la mtambo wa uteketezaji wa taka,na kufanya upanuzi wa bohari ya dawa ambayo yote imegarimu shilingi milioni 113.6.
Stori Na Kennedy Lucas, Manyara.
MWISHO.