MCHUNGAJI Florence Lanyero, wa kanisa la Rest Arena lilipo Gulu, Uganda, amekamatwa nyumbani kwake Februari 23, 2020, kwa kumiliki sare za jeshi na vifaa vingine vya kijeshi.
Jimmy Patrick Okema, msemaji wa polisi wa kituo cha Aswa, alisema wamemkuta akiwa na sare za jeshi na vifaa vingine vya kijeshi na hawajui kwa nini mtuhumiwa huyo anamiliki sare hizo.
Mchungaji huyo alianza kutafutwa baada ya kujipiga picha na kuziweka kwenye mitandao ya kijamii.
