KUFUATIA sakata la msanii wa Bongo Fleva, Aslay Isihaka Nassoro ‘Aslay’ kudaiwa kumdunda mzazi mwenzake anayejulikana kwa jina la Sonia na binti huyo kukiri kwa mdomo wake kwamba alipigwa lakini baadaye akakengeuka na kukanusha kupigwa, GLOBAL TV imezungumza kwa mara nyingine na familia ya binti huyo.
Akizungumza na Global TV, mama mdogo wa binti Sonia, amesema; “Sonia hajielewi, kwanza familia imemchoka, ana watoto watano lakini kila mtoto ana baba yake, tumechoka na tabia zake anazaa huko anakuja kutuachia watoto tuwalee, sasa awapeleke kwa baba zao, anadanganya ana miaka 25, ukweli ni kwamba ana miaka 30, tutaanika ukweli wote watu wamjue tabia zake chafu.”
Mama Sonia anasema kuwa mwanaye huyo ndiye alikuwa wa kwanza kumpigia simu akilia na kulalamika kuwa amepigwa na Aslay na kuwaomba ndugu zake wamfuate kwa Aslay. “Alinitumia mpaka location ya eneo alipokuwa, nikamkuta kweli amepigwa, tukampeleka polisi aipofika pale akaanguka na kuzirai.”
