×

Mangula Abainika Kuwa na Sumu Mwilini – Video

JESHI la Polisi Kanda ya Dar es Salaam, kupitia kwa Kamanda wake, SACP Lazaro Mambosasa, limesema baada ya uchunguzi wamebaini kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) – Bara, Philip Mangula,  ana sumu mwilini.

 

Akizungumza leo Machi 9, 2020 na Waandishi wa Habari, Kamanda Mambosasa amesema kuwa taarifa hizo walizipata Februari 28,2020, hii ni baada ya Mzee Mangula kudondoka ghafla katika ofisi ndogo zilizopo Lumumba mara baada ya kumaliza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu Taifa, iliyokuwa ikijadili mambo mbalimbali ikiwemo adhabu kwa wanachama wake watatu.

“Katika taarifa hiyo tulielezwa kwamba, Mzee Mangula alipelekwa Muhimbili na kulazwa ICU. Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ikishirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na Taasisi mbalimbali imebaini kwamba ndani ya mwili wa mzee Mangula kulipatikana na sumu.
“Uchunguzi kuhusu tuhuma ya sumu hiyo ilivyoingia mwilini upelelezi bado unaendelea. Kwa yeyote atakayebainika kupanga, awe ndani ya CCM, mwanafamilia ama Serikalini hatua kali zitachukuliwa dhidi yake, SACP Mambosasa.
Aidha, Kamanda Mambosasa amesema kuwa upelelezi kuhusu namna ambavyo sumu hiyo iliingia mwilini bado unaendelea, na Jeshi hilo halitasta kuchukua hatua kali kwa mtu yeyote atakayebainika kuhusika na uhalifu huo

Februari 28, mwaka huu, kiongozi huyo wa chama tawala alianguka ghafla na kupelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo alilazwa ICU kwa matibabu.

 

PHILIP MANGULA ALIWEKEWA SUMU, MAMBOSASA AZUNGUMZA – “JAMBAZI AMEKAMATWA”

Leave a Comment