×

Guardiola Aishangaa Man U

KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola, ameishangaa Manchester United kwa kuwa nyuma mno kiviwango dhidi ya City na kwamba hakutarajia hali ingekuwa hivyo wakati alipojiunga Etihad.

 

City na United zilimaliza zikiwa sawa kwa pointi 66 wakati Guardiola na Jose Mourinho walipotua Manchester mwaka Tangu hapo, City wameshaiacha kwa mbali sana United.

 

Msimu uliopita walimaliza wakiwa pointi 32 mbele ya United na kabla ya mchezo wa jana, walikuwa mbele yao kwa tofauti ya pointi 15 msimu huu.

 

“Sikutarajia kuwa na pengo kubwa la ponti kati yetu katika miaka hii mitatu au minne,” alisema Guardiola.

 

“Sina shaka juu ya ubora wa United na ninamkubali kocha (Ole Gunnar Solskjaer). United inapambana kuwa bora na kuwakaribia wapinzani wao walio juu yao lakini Manchester City nayo inataka kuwa bora zaidi.”

 

Katika hatua nyingine, kiungo Nemanja Matic amefanikiwa kuongeza mkataba Manchester United kufuatia kuwa na kiwango bora kwa siku za hivi karibuni chini ya Solskjaer.

 

Mkataba wa kiungo huyo, 31, ulitarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu na awali ilionekana kama anaweza kusepa kabla ya kiwango chake kuimarika kuanzia Desemba.

“Tumeshakubaliana naye, kwa hiyo atabaki. Asilimia 100,” alithibitisha Solskjaer.

MANCHESTER, England

Leave a Comment