×

Mloganzila Yaanzisha Huduma Maalum ya Macho

Dkt. Bingwa Catherine Makunja.

KATIKA kuadhimisha Wiki ya Macho Duniani ambayo hufanyika kila wiki ya pili ya mwezi Machi, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili iliyopo Mloganzila imefanya zoezi la upimaji wa bure wa presha (shinikizo)  ya macho ambapo takwimu zimeonyesha katika watu 65 watu tisa wamebainika kuwa na presha.

Dkt. Bingwa Judith Mwende.
Daktari akiwa kazini.

Wote waliobainika kuwa na tatizo hilo walipatiwa matibabu ya bure huku wengi wakipangiwa kuendelea na dozi.

Akizungumza na wanahabari, Daktari Bingwa wa Macho, Catherine Makunja,  aliwaomba wananchi kupima afya yao ya macho mara kwa mara ili kama kuna tatizo litakalobainika mapema iwe rahisi kulikabili.

Foleni ya upimaji ikiendelea.

Naye Daktari Bingwa mwingine, Judith Mwende, aliwasisitiza wananchi kufanya hivyo na kusisitiza kuwa presha ya macho inaweza kukusababisha upofu wa ghafla bila kutegemea.

Mwananchi aliyepimwa akisifia huduma alizopewa.

Baadhi ya watu waliofika kupata huduma hiyo waliusifu uongozi wa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John  Magufuli kwa kuwawezesha kupata bure huduma hiyo ambayo gharama zake ni kubwa mno na watu  wengi walikuwa wanashindwa kuzimudu na kuishia kuwa vipofu.

Hospitali  ya Mloganzila.

HABARI:NEEMA ADRIAN

PICHA: RICHARD BUKOS/GPL 

Leave a Comment