×

Polepole Afunguka JPM Kumlipia Msigwa

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hamphrey Polepole, amesema uamuzi wa  mwenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli, kumlipia faini ya Sh 38 milioni mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa ili atoke gerezani haupaswi kuchukuliwa kisiasa.

 

Amesema alimlipia faini Msigwa kwa vile binti wa Magufuli ameolewa katika familia ya mbunge huyo.

 

“Nimekwenda kama msaidizi wa ndugu Magufuli, Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania kutekeleza kazi yake binafsi. Anatumwa nani? Hilo ni utashi wa anayetuma. Waliogeuza siasa ni wale wasiojua utaratibu na wanaoingilia mambo ya kifamilia. Furaha ni kuwa ndugu yuko huru ametoka gerezani!” amesema Polepole.

 

Jana Alhamisi Machi 12, 2020, Magufuli, kupitia wasaidizi wake, alilipa  kiasi hicho cha fedha baada ya  ndugu wa Mchungaji Msigwa kuchangishana Sh. milioni 2 milioni na Magufuli kuongeza Sh. milioni 38 ili kukamilisha Sh40 milioni alizotakiwa kulipa mbunge huyo.

 

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on

Leave a Comment