
WAKAZI wa Jiji la Dar, maeneo ya Manzese, Magomeni, Kigogo-Sambusa, Buguruni na vitongoji vyake Machi 13, 2020 walipitiwa na kikosi cha mauzo na usambazaji cha magazeti ya Championi ambacho kilikuwa kikiinadi Bahati Nasibu ya Baba Lao ambayo mshindi anatarajiwa kuondoka na gari jipya aina ya FunCargo.
Akiinadi Bahati Nasibu hiyo, Mkuu wa Idara ya Masoko ya Magazeti ya Global, Anthony Adam, aliwahamasisha wananchi hao kununua magazeti ya Championi na Spoti Xtra ili kushiriki Bahati Nasibu hiyo.

Akiwaelekeza jinsi ya kushiriki bahati nasibu hiyo, Anthony aliwaambia: “Unachotakiwa kufanya ni kununua magazeti hayo na kukata kuponi iliyopo ukurasa wa pili na kujaza jina lako, namba yako ya simu, anwani yako na umri wako.


“Hapo utakuwa umemaliza kujaza kuponi hiyo na unachosubiria ni siku ya kuchezeshwa bahati nasibu hiyo”.
Sambamba na kujishindia gari, Anthony amesema kuna zawadi nyingine nyingi ambazo zitatolewa kila mwezi kuelekea kwenye droo hiyo ya kujishindia gari.
Alizitaja zawadi hizo kuwa ni pamoja na simu za mkononi za kisasa almaarufu kwa jina la Smart Kitochi na nyinginezo.


Na Richard Bukos