MUUNGANO wa Ulaya umepiga marufuku wasafiri kutoka nje ya muungano huo kwa siku 30 katika hatua ambayo haikutarajiwa ya kufunga mipaka yake kufuatia mzozo wa kuzuka ka tatizo la coronavirus.
Hatua hii inayahusu mataifa 26 wanachama wa EU na Iceland, Liechtenstein, Norway na Uswiss. Raia wa Uingereza hawataathiriwa na hatua hiyo.
Marufuku hiyo inatolewa huku idadi ya vifo vinavyotokana na mlipuko wa coronavirus ikiendelea kuongezeka katika nchi za Italia, Hispania na Ufaransa ambayo imeweka masharti makali ya kuzuia shughuli za umma na kuwataka raia wasalie majumbani mwao.
Ulaya imeathirika vibaya na virusi hivyo ambavyo vimewauwa watu 7, 500 duniani.
Wakati huohuo mashindano ya kombe la Euro 2020 yameahirishwa kwa muda wa mwaka mmoja.
Virusi vya corona vimewaathiri zaidi ya watu 185,000 kote duniani, kwa mujibu wa Shirika la Afya duniani (WHO).

