×

TANZIA: Aurlus Mabélé Afariki kwa Kansa na Corona

STAA na nguli wa muziki wa Soukous kutoka Jamhuri ya Congo, Aurlus Mabélé,  amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 67 nchini Ufaransa, baada ya kuugua kansa kwa muda mrefu na kukumbwa na maambukizi ya virusi vya Corona.

Mwanamuziki huyo aliyezaliwa akijulikana kama Aurélien Miatsonama mwaka 1953 jijini Brazzaville wilaya ya Poto-Poto aliuendeleza mtindo wa soukous na kujulikana kama Mfalme wa Soukous.

Miongoni mwa nyimbo zilizompa umaarufu ni pamoja na  Extra Ball, Embargo na Liste Rouge.

 

Leave a Comment