×

Bernard Morrison Apelekwa Ufukweni

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison,amebadilishiwa program na kocha wake, Luc Eymael ambapo kwa sasa anafanya mazoezi ufukweni.

 

Awali Morrison alikuwa akifanya mazoezi nyumbani tu katika kipindi hiki cha ligi kusimama kutokana na uwepo wa Virusi vya Corona, ambapo benchi la ufundi la Yanga liliwapa wachezaji wake wote program za kufanya wakiwa nyumbani.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Morrison amesema: “Awali baada tu ya ligi kusimama, nililazimika kununua vifaa vyangu binafsi vya mazoezi na nikawa ninafanya mazoezi ya asubuhi na jioni nikiwa nyumbani, lakini sasa hivi kocha kaniongezea kwa kunitaka nihakikishe napata hata kipindi kimoja cha asubhi au jioni cha kufanya mazoezi ufukweni.

“Baada ya kuanza program hiyo, naona kuna kitu kikubwa kinaongezeka kwangu maana hii imekuwa kama ‘pre-season’ kwangu kwani nilichelewa kuungana na wenzangu na nilikuwa nimekaa tu nyumbani zaidi ya mwaka mzima.”

Leave a Comment