×

Baba Mbaroni kwa Akidaiwa Kubaka Watoto Wake Wawili Mapacha – Video

JESHI la Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya limashikilia mkazi wa mtaa wa Rebu Shuleni, mjini Tarime mkoani Mara, Marwa Mwita kwa kutuhuma za kuwabaka watoto wake wawili wa kwambo wenye umri wa miaka 13, wakati mama yao hayupo.

 

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kuwatendea unyama huo watoto hao ambao ni mapacha (majina yao tumeyahifadhi) na wanafunzi ikiwa ni baada ya Serikali kufunga shule zote nchini kwa hofu ya maambukizi ya ugonjwa wa Covid 19 unaosababishwa ba virusi vya Corona.

 

Watoto hao ambao wanasoma Darasa la Tano katika (jina la shule tumelihifadhi) wilayani Tarime ambapo wamedai Baba yao wa kambo ambae anaishi na mama yao kwa sasa amekuwa akiwafanyia vitendo hivyo vichafu pindi jamaa huyo anapoona mwanya wa mkewe kutokuwepo nyumbani huku akiwatolea vitisho.

 

Baba mzazi wa watoto hawa amedai kumfuma mume mwenzake huyo na kwamba kitendo cha kuwageuza watoto wake kama wake zake huku mama yao naye akiendelea kuwa na mahusiano kunaleta picha mbaya ambapo kwa uapade wa mama yao akikiri uwepo wa madai hayo dhidi ya watoto wake.

 

Marwa ambaye anatuhumiwa kuwabaka watoto hawa amekanusha kuhusika na vitendo hivyo vya ubakaji na kuwa aliwataka wazoe uchafu ndipo ilipotengenezwa mbinu mbaya kwake.

 

Wakithibitisha kutokea kwa vitendo vya ubakaji Dhidi ya watoto hao Samson Chware ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Rebu Shuleni na Mtendaji wa Kata ya Turwa, Boniphace Mzurikwao wameiomba viongozi pamoja na mashirika yanayotetea na kupinga vitendo vya ukatili kuingilia kati .

Jeshi la Polisi Kanda maalumu Tarime na Rorya limethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo watuhumiwa pamoja na walalamikaji wamepelekwa katika kituo kikubwa cha Polisi Bomani mjini Tarime kwa maelezo zaidi.

 

 

Leave a Comment