×

Shamsa: Corona Imenituliza Nyumbani

STAA wa filamu nchini, Shamsa Ford amesema ugonjwa wa Covid19 umemfanya atulie nyumbani tofauti na hapo awali.Akichezesha taya na Amani, Shamsa alisema kuwa kwa sasa ametulia tu nyumbani mpaka hapo hali itakapokuwa sawa hata biashara zake za madera ameacha kwa hofu ya ugonjwa huo unaosababishwa na virusi vya Corona.

 

“Nilizoea muda mwingine kutoka tu ili kwenda kupoteza mawazo, nilikuwa naweza kwenda beach au hata nje ya nchi ili mradi nikale bata tu, lakini kwa sasa sitoki mpaka hili janga liishe.

 

 

Yaani hapa hamna namna, lazima tujilinde sisi na familia zetu ili uishe maana ukiisha tutaendelea kula bata kama zamani, kikubwa ni kuvumilia tu,” alisema Shamsa.

Leave a Comment