×

Solskjaer Aamini Rashford ni Bora Kwa Kane

KOCHA wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amesema kuwa ana furaha kwa kuwa klabu yake haikutumia pauni milioni 200 kumsajili Harry Kane.

 

Kocha huyo amesema kuwa anaamini kuwa uwezo wa mshambuliaji wake wa sasa Marcus Rashford ni bora kuliko mshambuliaji huyo wa Tottenham Hotspur.Imekuwa ikielezwa mara kwa mara United, wanataka kumsajili mshambuliaji huyo, lakini dili hilo limekuwa likigoma.

 

Hata hivyo, Gazeti la The Sun, limeripoti kuwa Solskjaer amekuwa akifurahia kitendo cha United kumkosa mchezaji huyo na kusema kuwa anaamini Rashford kwake ni bora zaidi na hawahitaji mshambuliaji wa bei ghali kiasi hicho.

Rashford, yupo nyuma ya Kane kwa miaka minne, lakini alikuwa mmoja kati ya wafungaji mahiri kwenye timu ligi hiyo baada ya kufunga mabao 19 kabla hajapata majeraha ya nyama za nyuma za paja msimu huu.

 

 

Kane ana mkataba na Spurs mpaka 2024, lakini bado inaelezwa United wanaweza kumsajili kwenye usajili wa majira ya joto. Nahodha huyo wa England ameshindwa kutwaa ubingwa wowote na Spurs tangu alipoanza kuichezesa akiwa mdogo.

Leave a Comment