×

Tanzia: Mkuu wa Uhamiaji Mkoani Kagera Afariki Dunia

MKUU wa Uhamiaji mkoani Kagera, Pendo Butenghe, amefariki usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Rufaa Mkoa ya Bukoba, baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Akizungumza na mwandishi wetu, Kaimu Mkuu wa Uhamiaji Kagera, Thomas Fush, amesema kuwa marehemu alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya kushuka sukari mwilini.

Amesema wanasubiri mwongozo wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa na makao makuu ya uhamiaji kujua taratibu za msiba na maziko.

Leave a Comment