×

Kagame Amfuta Kazi Waziri wa Mambo ya Ndani

RAIS wa Rwanda, Paul Kagame, amemuondoa madarakani Waziri wa Mambo ya Ndani, Jenerali Patrick Nyamvumba, kutokana na masuala ya uwajibikaji yanayofanyiwa uchunguzi.

 

Kutokana na taarifa iliyotolewa na Waziri Mkuu, Dkt. Edouard Ngirente, Jenerali Nyamvumba ametakiwa kuripoti Makao Makuu ya Jeshi kusubiri uamuzi zaidi.

 

Nyamvumba ni waziri wa tano kuondoshwa katika Baraza la Mawiziri  mwaka huu, akitanguliwa na Waziri wa Afya, Dkt. Diane Gashimba na Waziri wa Katiba na Sheria, Evode Uwizeyana.

 

Wengine walioondoshwa katika nafasi za uwaziri kwa mwaka huu ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Olivier Nduhungirehe  na Waziri wa anayehusika na Elimu ya Msingi na Sekondari, Isaac Munyakazi.

 

Awali, Nyamvumba alikuwa Kamanda Mkuu (Army Chief’) wa Jeshi la Rwanda tangu 2013 hadi 2019.

Leave a Comment