Spika wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai leo Mei 6, 2020 amewataka wabunge wa Chadema kurudi haraka bungeni siku ya kesho Mei 7, 2020.
Spika ndugai amesema endapo mbunge atakaidi agizo hilo la kurudi bungeni basi itawalazimu siku watakayo rudi wawe na cheti kinachoonesha kuwa wamepima ugonjwa wa Corona na majibu yake na kurudisha pesa walizolipwa ambazo ni posho za vikao la sivyo hatua zaidi zitachukuliwa.