×

JPM: Hatukuwa na Ebola, wala hawara yake Ebola – Video

 

RAIS John Magufuli  ameeleza namna alivyomfuta kazi aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa Tanzania (NIMR), Dkt. Mwele Malecela baada ya kutangaza uwepo wa ugonjwa wa Zika nchini Tanzania.

 

Akizungumza leo Ijumaa, Juni 5, 2020, katika Mkutano Mkuu wa Chama Cha Walimu Tanzania unaofanyika katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma,  amesema Watanzania wasitishwe wala wasiwe na hofu kuhusu Ugonjwa wa Corona kwani unaelekea kuisha kabisa.

 

“Wakati tunaingia madarakani tuliambiwa Tanzania kuna ugonjwa unaitwa Zika, aliyetangaza na aliyetumiwa kutangaza nikamfukuza kazi, bahati mbaya ni Mgogo, baada ya kumfukuza kazi siku chache akateuliwa na waliomtuma akatangaze kuna Zika akapewa Ukurugenzi.

 

“Baada ya kumfukuza yule Mgogo aliyesema Tanzania kuna Zika na waliomtuma wakamteua kuwa Mkurugenzi, mpaka leo miaka karibu mitano hapajawahi kuwa na kesi ya Zika hapa Tanzania.

 

“Baada ya uzushi wa Zika kupita na nilipomfukuza kazi aliyesema kuna Zika,tukakaa baadaye tukaambiwa kuna Ebola, walijua wakisema tuna Ebola watalii hawatokuja, tukasema sisi hatuna Ebola, wala mjukuu au hawara yake Ebola, na kweli hatujaona mgonjwa amekufa kwa Ebola Tanzania,” amesema.

Leave a Comment