
JESHI la polisi mkoa wa Dodoma Juni 12, 2020 limetoa taarifa mpya kuhusiana na shambulio la Mbunge wa Hai, ambaye ni mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, lililotokea siku chache zilizopita akiwa nyumbani kwake jijini Dodoma.
“Ushahidi kutoka eneo la tukio unaonesha kulikuwa na watu ambao kwa namna yoyote wangeweza kusikia makelele yaliyopigwa na Mbowe kuomba msaada, au kumuona bila kizuizi akishambuliwa, lakini hakuna hata mmoja aliyesikia kelele au kumuona akishambuliwa.
“Uchunguzi wetu umethibitisha kuwa siku Juni 8, 2020 Mbowe alitembelea sehemu za starehe zinazouza vileo na kupata kinywaji. Hata alipofika hospitalini alionekana akiwa katika hali ya ulevi chakari kiasi cha kushindwa kutamka maneno sawa sawa.”- Jeshi la Polisi Tanzania.
