
UMESIKIAmengi kuhusiana na kiungo mwenye kasi wa Yanga, Bernard Morrison kutoka Ghana. Kwamba kuna fedha dola 5,000 alipelekewa na wakala aliyemuambia kwamba zimetolewa na viongozi wa Simba.Hii ilisikika katika sauti yake iliyovuja mitandaoni na ikaelezwa alichukua.
Lakini kumekuwa na mengi yanazungumzwa kuhusiana na mkataba wake mpya kama kweli upo ni ule wa miezi sita au ana mpya wa miaka miwili!Ili kupata majibu sahihi ya hilo, ni Morrison pekee ndiye anaweza kutoa majibu na Championitumefanikiwa kumpata na kufanya naye mahojiano maalum ambayo yanafanywa na gazeti hili la Championi kwa kushirikiana na Global TV Online.