×

Sheva Awataja Kagere, Bocco Simba SC

KIUNGOmshambuliaji wa Simba, Miraji Athuman ‘Sheva’ amebainisha kuwa kwake hachagui straika wa kucheza naye kati ya Meddie Kagere na John Bocco kutokana na yeyote anayepangwa naye hucheza vizuri.

 

Sheva amesema kwamba kwake haangalii ni straika gani ambaye anapangwa kucheza naye kwa sababu amekuwa akielewana na kila mchezaji wanayecheza sambamba.

 

Kiungo huyo mwenye mabao sita, amesema kwamba kwake hamchagulii kocha wake Sven Vandenbroeck mtu wa kumpanga naye sambamba kwa sababu wamekuwa na uelewano mkubwa na straika yeyote ambaye anapangwa naye.

“Kuhusu kucheza na Bocco au Kagere, kwangu yeyote kati yao hakuna tatizo lolote kucheza nao kwa sababu tunafanya vizuri tukiwa uwanjani.

 

“Sichagui wa kucheza naye, yeyote anayepangwa basi tutashirikiana vizuri kufanya timu ipate matokeo yale mazuri na yatakayowaburudisha mashabiki wetu,” alisema Sheva.

Stori: Said Ally, Dar es Salaam

 

View this post on Instagram

 

Hapa Kazi Tu na Tanzania ya Viwanda ndiyo kauli mbiu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli na katika kumuunga mkono kiongozi huyo wa nchi, Taasisi ya Sinon Institute of Education, inatoa mafunzo yanayoweza kumfanya mhitimu akapata ajira kirahisi kwenye viwanda mbalimbali nchini. – Taasisi hiyo inatajwa kuwa kisima cha maarifa kutokana na jinsi inavyoweza kumuandaa mwanafunzi, kuanzia ngazi ya chini kabisa na kumfanya awe na thamani kubwa kwenye soko la ajira nchini. – Sinon Institute of Education iliyosajiliwa na serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatoa elimu kuanzia masomo ya elimu ya awali, msingi, sekondari, vyuo vya ualimu na mafunzo ya ufundi studi (TTC na VTC) ambayo yanawajengea wahitimu uwezo wa kujiajiri au kuajiriwa kwa maendeleo ya taifa. – Taasisi zilizopo chini ya Sinon Institute of Education ni pamoja na Healsun Pre and Primary School iliyopo jijini Arusha ambayo inatoa elimu kuanzia ‘baby class’, ‘middle class’, pre unit na darasa la kwanza hadi la saba. – Healsun inatoa nafasi kwa wanafunzi wa kutwa sambamba na wale wa bweni, kwa ada nafuu kabisa ya shilingi 480,000 kwa wanafunzi wa kutwa na shilingi 1,200,000 kwa wale wa bweni ambapo mzazi anarahishiwa ulipaji wa ada ambapo anaweza kulipa kidogokidogo kwa awamu nne. – Taasisi nyingine ni Healsun Technical Secondary School iliyopo jijini Arusha ambayo ni shule ya sekondari ya ufundi, inayotoa elimu kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne pamoja na ufundi. – Mbali na kupata elimu ya sekondari, lakini pia mwanafunzi atapata fursa adhimu ya kusoma Civil Engineering na Electrical Engineering kwa ada nafuu kabisa ya shilingi 1,540,000 ambayo mzazi anaweza kulipa kidogokidogo kwa awamu nne. Sinon Teachers College iliyopo Sekei jijini Arusha ikiwa na tawi jingine lililopo Kimara Temboni jijini Dar es Salaam, ni taasisi nyingine iliyopo chini ya Sinon Institute of Education, ambayo ni inatoa mafunzo ya ualimu na ufundi stadi. Kozi zinazotolewa na Sinon Teachers College ni ualimu wa awali (early childhood), ualimu wa msingi daraja la tatu (grade 3A) na diploma ya ualimu wa

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on

Leave a Comment