STAA wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu amesema kuwa anajijua kuwa ana miguu mibaya, lakini hiyo isiwafanye watu kuwa ndiyo fimbo ya kumchapia.
Akizungumza na Risasi Vibes, mrembo huyo alisema kwamba hakuna binadamu mkamilifu hapa duniani na Mungu hawezi kukupa vyote, hivyo yeye amekubali kunyimwa miguu mizuri.
“Unajua nimechoka na maneno ya watu wa mitandaoni, kila siku wanakesha kuisema vibaya miguu yangu, ukute ya kwao ni mibaya yangu ina afadhali, halafu Mungu hakupi vyote, lazima kuna ambacho atakunyima ili na wengine wapate, ndivyo alivyofanya kwangu, najua nina miguu mibaya, ila sitaki kuendelea kusemwa,” alisema Wema.
STORI | Memorise Richard, Risasi