
MSANII wa filamu za Kitanzania, Mariam Ismail ‘Mama Kubwa’ hivi karibuni ushosti wake na staa wa filamu Irene Uwoya umebadilika na kuwa mtu na wifi yake baada ya kuchumbiwa na mdogo wa pekee wa staa huyo aitwaye Babuu.
Akizungumza kwa furaha, Uwoya alisema kuwa kitu kilichotokea kwa yeye na Mariam, ni cha bahati sana kwani amepata wifi rafiki, ndugu ambao wanajuana kwa muda mrefu, hivyo anayeingia kwenye familia yao ni kama ndugu.
“Kwa kweli ni furaha kubwa kumpata wifi ambaye ni rafiki na ni kila kitu kwenye maisha yangu yanayonizunguka kwa sababu nilimpenda sana kama rafiki na sasa ni wifi yangu kwa mdogo wangu wa pekee kabisa,” alisema Uwoya.
Kwa upande wake Mariam, alisema anamshukuru sana Mungu kumpata mtu ambaye anampenda kwa dhati na kuingia kwenye familia ambayo anaipenda sana na ameishi nayo kwa muda mrefu.