×

Kilichotokea Dodoma Leo Mwinyi Akipitishwa Kuwania Urais – Video

MKUTANO wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wamempitisha Dkt. Hussein Ali Mwinyi Kuwa Mgombea wa urais wa Zanzibar kupitia chama hicho. Mkutano huo umefanyika leo Julai 10, 2020 katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma chini ya Mwenyekiti wa chama hicho Rais Dkt. John Magufuli.

 

“Jumla ya wanachama 32 wamejitokeza kuwania urais (Jamhruri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar) wakiwemo wanawake 5 na wanaume 27, lakini mwanachama mmoja aitwaye Hussein Ibrahim Makungu aliamua kujitoa katika mchakato huo na kubaki wanachama 31.

 

“Majina matatu ya wanachama wa CCM yaliyopendekezwa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwenye mchakato wa kuwania urais Zanzibar ni; Khalid Salim Mohammed, Dkt. Husseihn Ally Hassan Mwinyi na Ndg. Shamsi Vuai Nahodha,” amesema Dkt. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa CCM Taifa.
“Haikuwa kazi rahisi, tumepitia mengi na mengi mazuri na mabaya yamesemwa, lakini leo jahazi letu limefika Pwani. Niwahakikishie atakayeshinda hapa leo ndiyo atakuwa Rais wetu.” – Prof. Makame Mbarawa, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Dodoma.
“Watu wakitaka kupitisha kampeni zao wanaweza kusema wametumwa na huyu au huyu ni chaguo la yule, kama mimi walikuwa wakisema Prof. Makame Mbarawa ni chaguo langu, nimekuja nimembeba, sasa sijui leo watazungumza nani?
“Waacheni wagombea washuhudie hesabu ya kura zao wenyewe, ndiyo maana vyombo vya habari tumeviachia wanaonyesha kila kitu kinachoendelea kuhusu uchaguzi huu hapa ndani. Hata vyama vingine wajifunze kupitia kwetu kwamba CCM inayo Demokrasia ya kweli.” -Rais Magufuli, M/Kiti wa CCM

Akitangaza matokeo ya kura zilizopigwa na wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM Spika Job Ndugai, amesema waliopigiwa kura ni Shamsi Vuai Nahodha aliyepata kura 16, Dkt Khalid Salum aliyepata 19 na Dkt. Hussein Mwinyi aliyepata kura 129 sawa na asimilia 78.65 na hivyo kumfanya Dkt. Hussein Mwinyi kuchangulia kuwa mgombea urais wa Zanzibar.

 

Akizungumza mara baada ya kutagazwa kuwa mshindi Dkt. Mwinyi amesema kuwa amepewa heshima kubwa kwa kupata kura 129 na hiyo inaonyesha imani ya watu waliyonayo kwakwe na kuahidi kuwa atafanya kazi kwa kulitumikia Taifa kwa uwezo wake wote.

“Kinachonipa faraja ni kwamba tulikuwa 32 na hatimaye sasa niko mimi wezangu weote wako tayari kushirikiana nami kwa sasa hakuna timu Miwnyi wala timu nyingine bali kuna timu ya chama cha mapinduzi” amesema Mwinyi.

 

“Mzee wetu Abdulrahman Kinana amekiri hadharani kuwa alifanya makosa, ni uamuzi mgumu kukiri hadharani, alipewa adhabu ya miezi 18 na ameshatumikia miezi 4, hivyo ninawaomba tumsamehe, aje ajiunge nasi, lakini yule mwingine (Bernard Membe) amejitoa mwenyewe,” amesema Rais Magufuli.

 

Aidha, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimezindua rasmi na kuipitisha Ilani yake ya Uchaguzi ya Mwaka 2020 – 2025 leo Ijumaa, Julai 10, 2020, wakati wa Mkutano wa Halshauri Kuu ya CCM Taifa jijini Dodoma.

 

Leave a Comment