×

Breaking News: Rais Magufuli Atengua Uteuzi wa RC Makonda

Rais Dkt. John Magufuli amemteua Aboubakar Kunenge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar akichukua nafasi ya Paul Makonda. Kabla ya uteuzi huo, Kunenge alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar. Leo Julai 15, Makonda amechukua fomu kuomba ridhaa ya kuwania Ubunge, Jimbo la Kigamboni.

Mkuu moya wa Mkoa wa Dar, Aboubakar Kunenge.

Vile vile, Rais Magufuli amemteua Joseph Mkirikiti kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara kuchukua nafasi ya Alexander Pastory Mnyeti. Kabla ya uteuzi huo, Mkirikiti alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang mkoani humo.

 

Leave a Comment