×

WHO Kufanya Utafiti Dawa Mitishamba za COVID-19

SHIRIKA la Afya Ulimwenguni (WHO) na kituo cha udhibiti wa magonjwa barani Afrika (CDC) yameanzisha juhudi kuangalia uwezekano wa madawa ya mitishamba katika kupambana na janga la virusi vya corona.

 

Jopo hilo jipya la ushauri litaunga mkono nchi katika majaribio ya kitabibu, utafiti mwingine na utengenezaji wa dawa nyingine za kienyeji wakati hivi sasa janga likisambaa kwa kasi katika baadhi ya sehemu za bara la Afrika. Kesi zilizothibitishwa katika bara hilo zimekaribia kufika 750,000, zaidi ya nusu zikiorodheshwa nchini Afrika Kusini.

 

Taarifa ya WHO imesema dawa za asili, zina faida nyingi na bara hilo lina historia ndefu ya matumizi yake. Mkuu wa WHO barani Afrika, Matshidiso Moeti, amesema utafiti unapaswa kuwekwa katika misingi ya kisayansi.

 

Mataifa kadhaa yalionesha shauku baada ya Rais wa Madagascar kutangaza dawa ya mitishamba kama sehemu ya taifa hilo la kisiwani kupambana na janga la virusi vya corona.

Maambukizi duniani

 

Maambukizi ya virusi vya corona duniani yameongezeka kufikia  watu milioni 15 hadi siku ya Jumatano, kwa mujibu wa idadi iliyowekwa pamoja na shirika la habari la Reuters, wakati ugonjwa huo ukishika kasi hata wakati nchi bado zinaendelea kutofautiana katika jibu lao dhidi ya janga hilo.

 

Nchini Marekani, nchi ambayo ina idadi kubwa ya maambukizi duniani ikiwa na watu milioni 3.91 ya walioambukizwa, Rais Donald Trump alionya, kuwa huenda hali itakuwa mbaya zaidi kabla ya kutengemaa.

 

Nchi tano za juu ambazo zina maambukizi makubwa ni pamoja na Brazil, India, Urusi na Afrika kusini. Lakini idadi iliyowekwa pamoja na shirika la habari la Reuters inaonyesha ugonjwa huo unasambaa kwa kasi katika mataifa ya Amerika, ambayo yana zaidi ya nusu ya maambukizi duniani kote na nusu ya vifo. Duniani kote pia kiwango cha maambukizi hakionyeshi ishara ya kupungua kasi.

Leave a Comment