×

Mbelgiji Yanga Amtaja Luis wa Simba

BIG bosi wa Yanga, Luc Eymael amefunguka kuwa, ndani ya klabu hiyo kuna wachezaji hajawaona muda mrefu kutokana na kutoonekana mazoezini, huku akiwa hajui wako wapi.

 

Kocha huyo raia wa Ubelgiji, ameongeza kwamba wachezaji hao ni beki Ally Ally, Andrew Vicent ‘Dante’, Raphael Daud na Mohammed Issa ‘Banka’ ambao kwa muda mrefu walikacha kwenda mazoezini kabla ya kusafiri kwenda Morogoro na Iringa kwa ajili ya mechi za ligi kumaliza msimu huu.

Mbelgiji huyo ameliambia Spoti Xtra, kuwa: “Unajua kuna wachezaji kadhaa sijawaona mazoezini kwa muda wakiwemo Ally Ally, Dante, Raphael, Banka na Morrison.

 

Hawaji mazoezini na wanaonyesha kukosa uprofesheno.“Pia sifahamu ni wapi walipo na hiyo ilikuwa kabla ya kusafiri kumalizia mechi zetu hizi za mwisho wa ligi.“Siwezi kuwa na furaha kwa hali hiyo, hakuna timu ambayo itacheza vizuri bila ya wachezaji wake wote.

Watu wanatakiwa kujaji kwenye ukweli na siyo mambo ya kufikirika pale mambo yakiwa mabaya.“Fikiria Simba wangeweza kucheza bila Bocco (John), Miquissone (Luis), Wawa (Pascal), Mkude (Jonas), Kagere (Meddie) au Chama (Clatous)?” Alimaliza kocha huyo

Leave a Comment