×

Dkt. Abbas: WaTZ Mfike Uhuru Stadium Saa 12 – Video

MSEMAJI Mkuu wa Serikali, Dkt Hassan Abbas, amewataka Watanzania kujitokeza mapema katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, kesho ili waweze kupata fursa ya kumuaga kitaifa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa, kabla ya mwili wake kusafirishwa kupelekwa Lupaso, Masasi mkoani Mtwara kwa ajili ya mazishi.

 

Dk. Abbas ametoa mwongozo huo leo Julai 27, 2020, wakati akitoa ratiba ya kuaga mwili wa marehemu Mkapa ambapo amesema kuwa kwa kesho Jumanne Julai 28, shughuli zitaanza kwa misa itakayofanyika katika Kanisa la Immaculata na baadaye mwili utapelekwa Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya shughuli za kitaifa.

 

Aidha,  amewasihi wananchi kuwahi majira ya saa 12: 00 asubuhi katika Uwanja huo ili kupata fursa ya kusikiliza hotuba za viongozi mbalimbali. Pia  amesema kuwa misa ya maziko itasomwa pia Masasi Julai 29  itakayofanyika nyumbani saa 2 asubuhi na kuanzia saa 4 asubuhi shughuli za maziko zitaendelea.

Ameongeza kwamba  baada ya maziko Serikali itasikiliza hoja kuhusu suala la kubadilisha jina la Uwanja wa Taifa kuwa Uwanja wa Mkapa kwani ulijengwa kwa jitihada zake, na  ameongeza kuwa wanamichezo watamkumbuka kwa mchango wake katika sekta hiyo.

 

Leave a Comment