
MSANII wa Bongo Fleva anayekiwasha kwa sasa na Lebo yake ya Konde Gang Worldwide, Harmonize ameweka bayana kwamba mpenzi wake Sarah ambaye ni raia wa Italia ana ujauzito mkubwa na muda wowote anaweza kujifungua.
Harmonize amesema hayo wakati akipafomu kwenye Jukwaa la Jipoze Concert usiku wa kuamkia leo, Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, huku akianika siri nzito ya yeye kuachana na aliyekuwa mpenzi wake, Wolper baada ya kumfumania na meseji tofauti tofauti za wapenzi wake akiwemo mmoja aliyekuwa China na mwingine Burundi pamoja na kuomba penzi la Diamond Platnumz.
Akimzungumzia Wolper, Harmonzie amesema; “Nilipanga nisimwambie lakini anasema vingi, amekuwa akifanya interviews anamsema vibaya Sarah. Unavyomwita mwanamke wangu (Sarah) ambaye nampenda kwamba ni sponsor, kibinadamu inaumiza. Inaniumiza kumwita mpenzi wangu Sponsor ambaye punde si punde tunatarajia kuwa na mtoto kwa sababu tayari Sarah ni mjamzito,” amesema Harmonzie.