Serikali Yapokea Gawio La Shilingi Bilioni 17 Kutoka Benki Ya CRDB
BENKI ya CRDB Agosti 10, 2020 wamekabidhi jumla ya gawio la shilingi bilioni 17 kwa Waziri wa Fedha, Dkt. Philip Mpango ikiwa ni gawio kwa Serikali kuu, taasisi na mashirika yake kutokana na uwekezaji ndani ya benki yetu.
Mwaka huu tumetoa jumla ya gawio la shilingi bilioni 44.4 kwa Wanahisa wetu baada ya kupata faida ya shilingi bilioni 120.1 mwaka 2019 ikiwa ni ongezeko la asilimia 87 kulinganisha na faida ya shilingi bilioni 64 mwaka 2018.