TIMU ya Bayern Munich ya Ujerumani imeiadhibu timu ya Paris St Germain ya Ufaransa katika fainali kali ya kombe la ligi ya mabingwa Ulaya na kutawazwa mabingwa kwa mara ya sita katika mechi iliyochezwa Lisbon, Ureno.
Kingsley Coman ambaye alianza soka katika klabu ya PSG, alifunga goli la pekee kunako dakika ya 59 kwa kichwa kufuatia krosi iliopigwa na Joshua Kimmich na kuwaacha mabingwa hao wa Ufaransa wakihangaika dakika zilizobaki kutafuta ushindi wa kombe hilo.
Ulikuwa usiku wa furaha kwa mkufunzi wa Bayern, Hansi Flick, ambaye aliisaidia timu hiyo kupata kombe lake la pili msimu huu baada ya lile la ligi, alipochukua ukufunzi wa timu hiyo kufuatia kufutwa kazi kwa Niko Kovac mwezi Novemba.
Ulikuwa usiku mrefu kwa nyota wawili wa mabingwa hao wa Ufaransa, Neymar na Mbappe, ambao walishindwa kuonyesha umahiri wao na kujikuta wakifadhaishwa na kipa wa Bayern, Manuel Neuer, aliyepewa tuzo la mchezaji bora wa mechi wakati walipopoteza fursa za wazi.
Uchungu wa Mbappe uliongezeka katika kipindi cha pili wakati alipoonekana kuchezewa visivyo na Kimmich katika eneo hatari la goli, lakini hatua ya PSG kutaka kuzawadiwa penalti ilipuuzwa na kuiacha Bayern ikisherehekea kutawazwa kuwa mabingwa wa Ulaya.
Bayern walihitaji kushinda kombe hilo ambalo ni la sita kupitia uwezo wao na uthabiti wa kuzishinda timu nyingine lakini pia walionyesha ari ya kuwafadhaisha washambuliaji, Neymar na Mbappe.
Lakini sifa kubwa inafaa kumwendea kocha Flick ambaye ameiongoza Bayern kushinnda mara 21 mfulululizo, akiifufua timu hiyo na kuisaidia baada ya kufutwa kazi kwa Kovac mwezi Novemba huku klabu hiyo ikiwa katika mzozo.
Flick pia alionyesha uwezo wake wa kuchagua wachezaji akimuanzisha Coman badala ya raia wa Croatia, Ivan Perisic
BAYERN MUNICH MABINGWA WA ULAYA MARA SITA [6]
2020 🏆
2013 🏆
2001 🏆
1976 🏆
1975 🏆
1974 🏆
Bayern ndiyo timu ya KWANZA kushinda kila mchezo na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa #UCL
3-0 v Red Star
7-2 v Spurs
3-2 v Olympiacos
2-0 v Olympiacos
6-0 v Red Star
3-1 v Spurs
3-0 v Chelsea
4-1 v Chelsea
8-2 v Barcelona
3-0 v Lyon
1-0 v PSG







