The House of Favourite Newspapers

Simba: Tunawauzia Yanga Kessy

0

Hassan-‘-Kessy’-Ramadhani.jpgSaid Ally, Dar es Salaam

UONGOZI wa Klabu ya Simba umeuambia ule wa Yanga kuwa kama unataka kumsajili beki wao, Ramadhan Kessy, basi waende mezani kwa ajili ya kujadiliana nao pamoja na kupanga dau la kumuuza mchezaji huyo ambaye amekuwa akihusishwa kutakiwa na timu hiyo pamoja na Azam.

Kessy amebakiza miezi sita ya kuitumikia timu hiyo ya Simba inayonolewa na Muingereza, Dylan Kerr, ambapo kanuni za Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) zinamruhusu beki huyo kufanya mazungumzo na timu yoyote ile kwa ajili ya kujiunga nayo.

Akizungumza na Championi Jumatano, mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano cha timu hiyo, Haji Manara, alisema kuwa kama Yanga wana nia ya dhati ya kutaka kumsajili beki huyo, basi wafanye mpango wa kuonana na uongozi wa timu yao kwa ajili ya kuangalia namna gani wanaweza kumruhusu beki huyo kuhama ndani ya kikosi chao.

“Tunasikia tu kuwa wapinzani wetu, Yanga wapo katika mchakato wa kutaka kumsajili mlinzi wetu, Hassan Kessy, jambo ambalo sisi hatuna taarifa nalo zozote, kwani wao mpaka sasa hawajaleta barua rasmi ya kuthibitisha kuwa wana nia ya kumsajili beki huyo.

“Lakini kama itakuwa kweli wanamtaka Kessy basi tunawaambia waje kuonana na uongozi wetu na kuweka mjadala wa kuangalia tunaweza kumuuza mchezaji huyo kwa dau gani haswa na kama tukifikia makubaliano tutamruhusu aende kwani sisi hatuna utamaduni wa kumng’ang’ania mchezaji ila siyo kumfuata mchezaji huyo kimyakimya wakati wanajua bado ni mali yetu,” alisema Manara.

Leave A Reply