
MGOMBEA mwenza wa kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan, leo Septemba 11, 2020 amezungumza na wananchi wa Jimbo la Mahuta, Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara, kwenye mkutano wa kampeni wa CCM kijijini Mahuta, Mtwara, leo Septemba 11, 2020.
Wanachama 150 kutoka vyama vya ACT Wazalendo, CUF na Chadema wilayani Tandahimba, leo wamerudisha kadi za vyama vyao na kujiunga na CCM kwenye mkutano wa huo wa kampeni.




