RAPA maarufu nchini ambaye hivi karibuni alisainiwa na Lebo ya konde Gang chini ya Harmonize, amefunguka mengi kuhusu ushikaji wake na msanii huyo mpaka kufikia hatua ya kufanya kazi pamoja kwenye record label hiyo.
Country amesema hayo leo Jumatatu, Septemba 14, 2020, wakati akifanyiwa mahojiano na kipindi cha Bongo 255 kinachoruka kupitia +255Â Global Radio.
“Mimi ndo rapa wa kwanza Bongo kumiliki Noah, tena Noah yangu ni ya wana, wanapanda washkaji tu. Kwa hiyo Konde Gang kunipa zawadi ya gari wameniongezea, kwa sasa nimefikisha magari mawili.
 “Sijawahi kufanya kazi na msanii yeyeote wa WCB tofauti na Konde Boy, sishindwi kufanya kazi na msanii yeyote Tanzania, sababu wanauelewa muziki wangu, lakini napofanya kazi zangu naangalia nafanya na yupi ambaye nitafiti.
“Siku moja usiku niliishiwa mafuta kwenye gari likazimika, kila niliyempigia hapatikani, nikawaza nimpigie Harmonize sijui atanifikiriaje, nilipompigia alikuwa studio akaacha kazi zake, akaenda sheli na kidumu kuchukua mafuta akaniletea, akanipa na dola 50, Konde yuko peace sana, ni msanii anayejituma sana na anaiheshimu kazi yake,” amesema Country Boy.
