
Benki ya NCBA Tanzania Limited (NCBA) imefanya uzinduzi wa kihistoria wa matawi yao mawili mapya jijini Arusha leo tarehe 19 Septemba, 2020.

Matawi hayo mawili mapya ya Arusha ni Tawi la Clock Tower lililopo Fire Road, Jengo la TFA na Tawi la Sokoine lililopo Barabara ya Sokoine, Central Plaza ghorofa ya chini.

Benki ya NCBA ni muunganiko wa hiari kati ya NIC (T) Limited na CBA Bank (T) Limited ambapo huduma rasmi za taasisi hii mpya ya Kifedha zilianza Julai 8, 2020 baada ya idhini kutoka Benki Kuu ya Tanzania.
