×

Wabunge Wakataa Msaada wa Kondomu

WABUNGE nchini Malawi wamekataa kupokea msaada wa  kondomu zaidi ya 200,000 walizopewa na shirika moja la kutoa misaada. Mipira hiyo ilikuwa iwekwe katika vyoo vya majengo ya bunge.

 

Kiongozi wa wabunge wengi bungeni humo, Richard Chimwendo, amesema wabunge hawahitaji msaada huo kwa sababu wana uwezo wa kumudu bei ya kondomu.

 

Ripoti hiyo ilimnukuu kiongozi mmoja mbunge, Bi Chinsinga,  akisema kuwa bunge hutumia karibu mipira 10,000 ya kondomu kila mwezi na kwamba wakati mwingine “zinaisha”.  Hiyo ni kwa mujibu wa gazeti la Nation la nchini humo.

 

Hata hivyo, Naibu wa Spika, Madaliotso Kazombo, amekanusha madai haya na kutaka gazeti hilo kuomba radhi.

Leave a Comment