×

Dkt. Abbas Atembelea Studio za S2Kizzy Zilizovamiwa – Video

 

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas mchana wa leo tarehe 15 Oktoba, 2020 amefika katika studio za producer S2KIZZY ambazo usiku wa kuamkia leo kulitokea uvamizi ambapo watu kadhaa waliumizwa na uharibifu wa vifaa vya studio.

Baada ya kujionea hali halisi Dkt. Abbas amesisitiza watu kuiheshimu sanaa na kwamba sanaa ni kazi kama ilivyo kazi zingine  huku akiahidi kuwa polisi wanakamilisha uchunguzi ili haki itendeke.  “Tukio hilo liko polisi, nimeagiza uchunguzi ufanyike haraka na hatua kali zichukuliwe dhidi ya waliohusika na tukio hilo.”

Humphrey Polepole asikitishwa na Skizzy kuvamia, atoa kauli hii; “Tumepokea taarifa za kuvamiwa studio ya S2KIZZY ambako wasanii waliokuwa wakijiandaa kurekodi, wamepigwa na kufanyiwa vitendo vya unyanyasaji. Haikubaliki! Tumesema na Jeshi la Polisi kuchunguza tukio ili haki ipatikane na kuwachukulia hatua kali wavamizi. #Muzikinimaisha”

 

 

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on

Leave a Comment