Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam wanamshikilia Mtu mmoja kati ya 17 waliovamia Studio ya @s2kizzy kwa kujifanya Polisi jamii na ulinzi shirikishi usiku wa Oktoba 14, 2020 ambapo waliwakamata Wasani na kuwapeleka Polisi kituo cha kijitonyama na kuwafungulia kesi za uongo.
“Nimeagiza Wasanii hao waliokamatwa waachiwe huru mara moja na hilo genge la wahuni lisakwe, hao sio Polisi Jamii, hakuna Polisi Jamii wanaoweza kufanya kazi peke yao bila Baraka za Viongozi wa Serikali, nimeagiza wahusika wote 17 wakamatwe, Kiongozi wao tunae na msako unaendelea….”
View this post on Instagram
