×

Kaze Akomaa na Sarpong, Yacouba

KOCHA Mkuu wa Yanga,  Mrundi, Cedric Kaze, amewaongezea majukumu washambuliaji wake Michael Sarpong na Yacouba Songne ya kuwa makini katika kufunga mabao ambayo yatawapa pointi tatu hasa kwenye mechi zao za nje ya Dar.

 

Kaze ameongeza kwamba, mastraika hao wanatakiwa kuwa makini na nafasi hizo kwa sababu viwanja vingi vya mikoani haviwapi nafasi ya kutengeneza nafasi nyingi za kufunga.

 

Kocha huyo ameliambia Spoti Xtra, kuwa zoezi hilo wataanza nalo katika mechi zijazo za mikoani ili kuwa na uhakika wa kupata pointi tatu na si kubahatisha.

 

“Unajua mkoani kule viwanja havina ubora mzuri kwa hiyo inafinya nafasi ya kutengeneza mashambulizi mengi kwa mpinzani wako.

“Hivyo ni muhimu sana katika zile nafasi chache ambazo timu itatengeneza ni lazima tutumie kwa usahihi kwa ajili ya kuwa na uhakika wa kupata pointi tatu.

 

“Tukishindwa kufanya hivyo inatuweka kwenye mazingira magumu sana ya kupata kile ambacho tunakitaka, hivyo ni muhimu kwa wachezaji wangu kulizingatia hilo,” alimaliza Kaze.

 

SAID ALLY, Dar es Salaam

 

 

Leave a Comment