×

Vodacom Yazindua Huduma ya Duka Linalotembea

Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom PLC, Linda Riwa akizungumza kwenye uzinduzi huo.

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom PLC imezindua huduma ya Duka linalotembea ili kuwafikia wateja popote.

Uzinduzi umefanyika jana Jumatano katika Soko Kuu la Kariakoo Jijini Dar.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom PLC, Linda Riwa amesema katika duka hilo zitapatikana huduma zote zinazopatikana kwenye maduka mengine ya Vodacom PLC.

Linda Riwa na Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na Usambazaji, George Lugata (kulia) wakigonga ‘chiaz’ na wadau wengine kusherehekea uzinduzi huo.

Linda alizitaja huduma hizo kama vile kuuza simu na vifaa vyake, huduma za M-Pesa, usajili wa laini na mambo mengine.

Watoa huduma wa Vodacom PLC wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya uzinduzi.

Ameendelea kusema kuwa wameamua kufanya ubunifu huo kwa ajili ya kuwafikia kiukaribu wateja wao waliopo sehemu mbalimbali.

Muonekano wa duka hilo.

Katika hafla hiyo ya uzinduzi walikata keki na kugonga shampeni pamoja na umati uliokusanyika eneo hilo kushangilia uzinduzi huo.

Leave a Comment