×

Jamaa Aliyejifanya Katibu wa Kangi Lugola Afikishwa Mahakamani

Mtuhumiwa, Godfrey Haule (kulia) akiwa na askari kanzu wakati akishuka ngazi za Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam.

Mkazi wa jiji la Dar es Salaam, Godfrey Haule amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kujifanya yeye ni katibu wa aliyekuwa waziri wa Mambo ya ndani Kangi Lugola wakati akijua siyo kweli.

Akisoma hati ya mashtaka wakilii wa Serikali, Faraji Nguka amedai  kuwa mshtakiwa huyo ana mashtaka mawili ya kujifanya mtumishi wa umma na moja la kuomba rushwa.

Wakili Nguka amedai kuwa Oktoba 31,2018 maeneo tofauti ya jiji la Dar es Salaam mshtakiwa huyo alijifanya  ni katibu wa waziri wa Mambo ya ndani Kangi Ligola wa wakati huo.

Shtaka la pili inadaiwa Novemba 2018 maeneo hayo mshtakiwa huyo akiwa na nia ovu alijifanya ni Lucas Mdemu akijitambulisha ni katibu wa waziri wa Mambo ya ndani Kangi Ligola huku akijua siyo kweli kisheria.

Katika shtaka lingine inadaiwa kati ya Novemba 2 na 3, 2018 maeneo hayo mshtakiwa  akiwa pamoja na wengine ambao hawapo mahakamani hapo waliomba rushwa ya Sh 15 milioni Kwa Lucas Mdemu ili ayafiche makosa yake ya jinai kwa raia wa Jamuhuri wa Muungano.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo alikana na upelelezi bado haujakamilika. Hakimu Mkazi Mkuu,Yusto Ruboroga amesema mshtakiwa anatakiwa awe na wadhamini wawili ambao kila mmoja atasaini bondi ya Sh 5 milioni.

Aidha Mshtakiwa ametakiwa awasilishe fedha taslimu Sh7.5 milioni au apeleke hati ya mali isiyohamishika yenye thamani hiyo.

Mshtakiwa huyo ameshindwa kutimiza masharti hayo hivyo amepelekwa mahabusu na kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 27,2020.

Leave a Comment