×

Mwili wa Zipompa Ulivyopumzishwa Kwenye Nyumba Yake ya Milele

Aliyekuwa muigizaji wa filamu za Kibongo na mshereheshaji maarufu nchini, Gladys Chiduo maarufu kama Zipompapompa, mwili wake jana jioni ulipumzishwa kwenye nyumba yake ya  milele kwenye Makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Mazishi hayo yalihudhuriwa umati mkubwa wa waombolezaji wakiwemo mastaa wenzake huku washereheshaji na wasanii wa filamu za kibongo wakifurika zaidi.

Katika mazishi hayo watoto wa marehemu, Herry, Fadhili na Dada yao Enzelani waliongeza simanzi kwa waombolezaji wakati wakienda kuweka shada la maua kwenye kaburi la mama yao huku wakionesha huzuni iliyopenya mioyoni mwa waombolezaji.

Katika mazishi hayo upande wa serikali uliwakilishwa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Dkt. Kiango Kilonzo aliweka udongo na taji la maua kwenye kaburi la marehemu.

Wengine walioweka taji ni pamoja na msanii wa vichekesho Joti, Pierre Liquid na wengineo.

Zipompapomba enzi za uhai wake alisifika sana kwa ucheshi wake haswa alipokuwa kwenye kazi ya ushereheshaji jambo lililosababisha kuongezeka kwa wateja wake kila kulipokucha huku akihitajika kwenye uigizaji.

Zipompa alipatwa na umauti usiku wa kuamkia Jumatano iliyopita Novemba 10 mwaka huu baada ya kuzidiwa akiwa nyumbani kwake Mbweni jijini Dar na kukimbizwa Hospitali ya Rabininsia iliyopo Tegeta Dar.

Mwili ukipelekwa kaburini.
Watoto wa marehemu wakifarijiana.
Mchungaji Angela akiuombea mwili wa marehemu kabla ya kuzikwa.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu, Dkt. Kiango Kilonzo akitia udongo kaburini kuashiria kumuaga marehemu.
Watoto wa marehemu kutoka kushoto Fadhili Baraza, Enzelina Baraza na Herry Baraza wakiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu mama yao.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu, Dkt. Kiango Kilonzo aliyeiwakilisha serikali kwenye mazishi hayo akiweka shada la maua.
Steve Nyerere akilia wakati akiweka shada.
Joti akiweka shada.
Pierre Liquid akimuombea marehemu.
Anko Shamte ambaye ni mume wa Mama Diamond Platniumz naye akiwa mazishini hapo.
Baadhi ya Wasanii wa Bongo muvi makaburini hapo.
Mtangazaji wa Kipindi cha Mboni Talk Show, Mboni Masimba akiwa na simanzi tele.
Waombolezaji ni kama hawaamini kilichotokea.                                                                          HABARI/PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS /GPL

Leave a Comment