
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi kesho, Novemba 19, 2020, anatarajiwa kutangaza baraza la mawaziri katika hafla maalum itakayofanyika asubuhi.
Dkt. Mwinyi ameshamteua Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Dkt. Mwinyi Talib Haji.
Pia, ameshamteua Mkurugenzi Mkuu wa Shirika Ia Bandari Zanzibar, Nahaat Mohammed Mahfoudh na Katibu wa Rais, Suleiman Ahmed Salch.
Katika hatua nyingine Mwinyi amefanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya Mnazi Mmoja na kuutaka uongozi wa hospitali hiyo kuhakikisha watendaji wake wote wanatambulika kwa majina mara moja ili wanaokwamisha huduma wajulikane.
Akizungumza mara baada ya ziara hiyo, ameweka wazi kuwa ujio wake katika hospitali hiyo umetokana na taarifa kutoka kwa baadhi ya wagonjwa wanaofika kwenye hospitali hiyo ambao wanalalamika juu ya kutoridhishwa na huduma zinazotolewa hospitalini hapo.