×

Mwili wa Marehemu Wapotea Kwenye Jeneza, Wakutwa Nyumbani

WANANCHI wa Kijiji cha Kona Nne Wilaya ya Kaliua mkoani wa Tabora wameshangazwa na kurejea kwa mwili wa marehemu aliyefariki kwao na kusafirishwa kwenda Kahama na wakati wakijiandaa kwa mazishi mwili ukarudi kwa mazingira ya tatanishi Kijijini hapo.

 

Mwenyekiti wa Kitongoji cha King’wangoko Said Nzogola amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mwili huo umerudi, na kabla ya kuusafirisha kwenda Kahama ndugu wa marehemu walidai mahari ya binti yao.

 

“Waliondoka wameubeba na kaka yake kutoka tumbo moja alikuwepo na walipofika kule nao wakashangaa na baadae jione wakarudi kuchukua mwili tena na mwanzo kabla halijatokea tukio hilo walikuwa wanadai mahari shilingi Mil.1.5,” Said Nzogola.

Leave a Comment